SAVE THE CHILDREN YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI MKOA WA DODOMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAVE THE CHILDREN YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI MKOA WA DODOMA

Shirika la Kimataifa la Kuhudumia watoto la Save The Children kupitia mradi wake wa Lishe Endelevu unaolenga kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, wajawazito na wanaonyonyesha, vijana wa rika la balehe na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano limeadhimisha wiki ya Unyonyeshaji duniani mkoani Dodoma.
Kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children yamefanyika leo Agosti 7,2019 katika kijiji cha Kingale wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma. 
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Dodoma Benety Malima alisema maadhimisho hayo ya wiki ya unyonyeshaji ni sehemu ya utekelezaji wa mradi Lishe Endelevu unaofadhiliwa na Mfuko wa Watu wa Marekani 'USAID'.
Malima alitumia fursa hiyo kuwahimiza waajiri kwenye mashirika na taasisi mbalimbali kutenga chumba maalumu kwa ajili ya akina mama kuwan... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More