SAVE THE CHILDREN YAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SAVE THE CHILDREN YAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA

Shirika la Save The Children limekutana na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika mafunzo ya siku moja kwa ajili ya kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Novemba 19,2018 katika ukumbi wa Good Shepherd mjini Kahama, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Akifungua mafunzo,Macha aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.Alisema katika wilaya ya Kahama,halmashauri za Msalala na Ushetu zinaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni kutokana na mila na desturi kandamizi,umaskini,tamaa za mwili,mazingira pamoja na maendeleo ya teknolojia ambapo simu za mkononi zimekuwa zikiongeza tamaa kwa wanafunzi.
“Waandishi wa habari mna nafasi kubwa katika vita hii ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa mnawafikia watu wengi zaidi kupitia habari zenu,Lazima wadau wote tushirikiane kuto... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More