Sekta ya mifugo Kuchangia Asilimia 9 ya Pato la Taifa - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Sekta ya mifugo Kuchangia Asilimia 9 ya Pato la Taifa


Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatekeleza mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya mifugo unaotarajiwa kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa kutoka asilimia 6.9 hadi 9%.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega amesema bungeni jijini Dodoma kuwa, utekelezaji wa mkakati huo pia unatarajiwa kukuza sekta ya mifugo kutoka asilimia 2.8 hadi 5.2%.
Wakati anajibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvester Koka, Ulega amesema, mkakati huo una lengo la kupunguza na kuboresha mazingira rafiki na endelevu katika uzalishaji mifugo yenye tija kwa kuzalisha mitamba milioni moja kwa mwaka.
Wabunge wameelezwa kuwa mitamba hiyo itapatikana kutoka makundi ya ng'ombe wa asili kwa kufanya uhimilishaji. Koka alitaka kufahamu Serikali ina mpango gani kuboresha bidhaa za nyama nchini pamoja na mazao mengine yatokanayo na mifugo.
Ulega amesema, mkakati wa kuendeleza sekta ya mifugo utaimarisha upatikanaji wa uhakika wa maji, malisho na vyakula bora vya mifugo, utahamasisha matumizi ya ... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More