SEKTA YA UVUVI YAIMARIKA, BOTI YA DORIA YAHITAJIKA KUIMARISHA ULINZI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SEKTA YA UVUVI YAIMARIKA, BOTI YA DORIA YAHITAJIKA KUIMARISHA ULINZI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamiiUVUVI na uuzaji wa samaki katika soko la Feri jijini Dar es salaam umezidi kuimarika katika mchakato mzima wa uvuvi wa samaki wenye viwango vinavyotakiwa na uuzwaji wake sokoni umekuwa na tija.
Akizungumza na blogu ya jamii Kaimu Afisa Uvuvi wa soko la Feri Ahmed Mbarouk ameeleza kuwa upatikanaji wa samaki kwa sasa ni mzuri hasa kwa samaki wakubwa  na hata mauzo yamekuwa mazuri pia kutokana na ubora wa samaki wanaovuliwa kuwa na viwango.
Kuhusiana na kutokomeza uvuvi haramu Abdallah ameeleza kuwa kwa sasa hakuna matukio hayo ya wavuvi kutumia baruti kuvua samaki na hii ni baada ya kampeni waliyoiendesha na kufanikisha kukamatwa kwa nyavu haramu kubwa 14 aina ya kokoro ambazo ziliteketezwa.
Akieleza changamoto wanazokabiliana nazo kiutendaji Afisa uvuvi huyo amesema kuwa vifaa vya kazi hasa boti la doria limekosekana hali inayowapelekea kufanya doria kwa miguu licha ya kuwa na askari wa Suma JKT wanaosaidia na kueleza kuwa boti hilo likipatikana litawarah... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More