SERENGETI BOYS YAANZA VYEMA KOMBE LA CECAFA KUFUZU AFCON U17 2019 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERENGETI BOYS YAANZA VYEMA KOMBE LA CECAFA KUFUZU AFCON U17 2019

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TANZANIA imeanza vyema leo michuano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Burundi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Mabao ya Serengeti Boys katika mchezo huo wake huo wa kwanza wa michuano hiyo ijulikanayo kama CECAFA CAF Afcon qualifier yamefungwa na Kelvin John dakika ya 11 na Agiri Ngoda dakika ya 29, wakati la Burundi limefungwa na Edson Munaba dakika ya 20.
Wachezaji wa Serengeti Boys wakishangilia ushindi wao dhidi ya Burundi leo

Mchezo wa kwanza kabisa wa ufunguzi wa michuano hiyo, Rwanda iliichapa Sudan mabao 3-1 hapo hapo Uwanja wa Taifa.
Mabao ya Rwanda yamefungwa na Moise Nyarugabo dakika ya 30, Rodrigue Isingizwe dakika ya 33 na Jean Isimiwe dakika ya 89, wakati la Sudan limefungwa na Mohammed Badri dakika ya 71.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mchezo mmoja, kati ya Sidan Kusini na Djibouti kuanzia Saa 8:00 mchana. Ikumbu... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More