SERENGETI BOYS YAKUTWA NA ‘VIJEBA’ WAWILI…WAENGULIWA MICHUANO YA KUFUZU AFCON 17 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERENGETI BOYS YAKUTWA NA ‘VIJEBA’ WAWILI…WAENGULIWA MICHUANO YA KUFUZU AFCON 17

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NYOTA wawili wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Jafary Mtoo na Lenox Fred Chande ni miongoni mwa wachezaji 11 walioondolewa kwenye michuano ya kuwania kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Wachezaji hao wameondolewa baada ya zoezi la vipimo vya kuthibitisha umri (MRI) zoezi lililofanyika hospitali ya Muhimbili na kusimamiwa na madaktari wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ajili ya michuano hiyo ijulikanayo kama CECAFA CAF Afcon qualifier ambayo inaanza leo mjini Dar es Salaam.

Madaktari wa Hitech Sai Healthcare Centre, Ada Estate, Laila Khan na Baby Khan wakimfanyia vipimo mchezaji wa Serengeti Boys, Ben Anthony Starkie anayechezea Leicester City U16 ya England 

Wachezaji walioondolewa walikutwa wamezidi umri wa miaka 17 katika vipimo vya madaktari wa CAF iliyobadili mfumo wa mashindano ya kufuzu kwa AFCON U17 ambao ni Yaci... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More