Serikali Gabon yasema hali ni shwari, kufuatia jaribio la jeshi kutaka kuipindua serikali - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali Gabon yasema hali ni shwari, kufuatia jaribio la jeshi kutaka kuipindua serikali

Waziri wa mawasiliano nchini Gabon anasema wanajeshi waaminifu kwa serikali ya Rais Ali Bongo wamefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya serikali nchini humo.

Bw Guy-Bertrand Mapangou ameambia BBC kwamba wanajeshi wanne waliohusika katika jaribio hilo wamekamatwa na mwingine wa tano anasakwa.

“Hali ni tulivu. Polisi ambao huwa hapo wamerejea na kuchukua udhibiti wa eneo lote la makao makuu ya mashirika ya redio na runinga, kwa hivyo kila kitu kimerejea kawaida,” amesema.

“Walikuwa watano. Wanne wamekamatwa na mmoja yupo mafichoni na atakamatwa saa chache zijazo.”

Kundi la wanajeshi nchini Gabon lilikuwa limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi na kutangaza amri ya kutotoka nje.

Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita walikuwa wakishika doria katika barabara za mji mkuu Libreville.

Kwa mujibu wa BBC, Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo lilitangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More