Serikali Haijavunja Mkataba wa Wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya Juu - Prof. Ndalichako. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali Haijavunja Mkataba wa Wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya Juu - Prof. Ndalichako.

Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali imesema haijavunja mkataba wowote na wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu bali makato ya asilimia 15 kutoka kwenye mshahara ghafi wa mnufaika wa mkopo huo ni ya kisheria.

Hayo yameelezwa leo Bungeni, Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Mhe. Paschal Yohana Haonga juu ya kinachodaiwa kuwa Serikali imevunja mkataba kinyume na makubaliano kwa kuwa wakopaji walisaini mkataba wa asilimia 8 na siyo 15.

"Kilichofanyika mwaka 2016 katika marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Mikopo (SURA 178) ni kuiboresha sheria hii kwa kutaja kiwango mahsusi cha asilimia 15 kinachopaswa kukatwa kutoka mshahara ghafi wa mnufaika. Awali, kabla ya marekebisho hayo, kifungu cha 7(1) (h), kiliipa Serikali mamlaka ya kupanga kiwango cha makato na kubadilisha kiwango pale itakapoona inafaa," alifafanua Prof. Ndalichako.

Ameendelea kusema kuwa, Serikali inafahamu umuhimu wa kuwashirikisha wadau... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More