SERIKALI HAITAWAVUMILIA WANAOPOTOSHA WAKULIMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI HAITAWAVUMILIA WANAOPOTOSHA WAKULIMA


Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewataka Wakulima kutokusikiliza maneno ya barabarani ya wapotoshaji na badala yake waendelee kuiamini Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Gavana Shilatu aliyasema hayo Leo Jumatano Januari 9, 2019 alipokutana na kufanya kikao na  Wakulima wakubwa wa Korosho wanaoishi Kata ya Mihambwe.
Gavana Shilatu amewataka Wakulima kusimama imara na kuwapuuza wale wote wanaopotosha maana halisia ya zoezi la uhakiki wa Korosho kwa Wakulima.
*"Rais Magufuli ameonyesha nia ya dhati ya kutaka kumkomboa kiuchumi Mkulima wa Korosho. Zoezi la uhakiki linafanywa kuhakikisha Mkulima halisia ananufaika na jasho lake na sote tupuuze maneno  ya vijiweni. Serikali ipo kwa ajili ya kusimamia haki na jasho la Mkulima linamnufaisha Mkulima mwenyewe. Serikali haitawavumilia wanaopotosha Wakulima, wanaopotosha nia njema ya Rais Magufuli Kwa Wakulima."* alisema Gavana Shilatu.
Gavana S... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More