SERIKALI, HPSS WAZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI SHINYANGA KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI, HPSS WAZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI SHINYANGA KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA

Serikali mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Wadau wa afya (HPSS) wamezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ili waweze kupata huduma ya matibabu kwa gharama nafuu.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika leo Julai 16, 2019 kwenye kijiji cha Ilobashi kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa huo,Mhe. Zainab Telack, na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya CHF iliyoboreshwa ,Telack amewataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga wajiunge kwa wingi, ili pale wanapotatwa na magonjwa na kukutwa hawana fedha,kadi hiyo ya CHF itawawezesha kuwapatia matibabu bure bila ya kutoa gharama yoyote ile.Amesema kadi hiyo ya bima ya afya CHF iliyoboreshwa inakatwa kwa bei ya Shilingi 30,000 kwa kila Kaya, ambapo watatibiwa watu sita kwenye kaya moja kwa muda wa mwaka mzima, ambapo matibabu watayapa kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, wilay... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More