Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali Imetoa Kibali cha Ajira 15,000 Kuziba Pengo la Walioghushi Vyeti

NaLilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.SERIKALI imetoa kibali cha kuajiri watumishi wapya 15,000 ili kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi wa Umma waliobainika kughushi vyeti.
Hayo yameelezwa leo Bunge, Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Capt. (Msataafu) George Mkuchika alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Aida Khenani kuhusu mkakati wa Serikali wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliokumbwa na sakata la vyeti feki.
"Vibali vya kuajiri watumishi hao vimetolewa katika ngazi ya Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waajiri wote wameendelea kujaza nafasi hizo, " alisema Mhe. Mkuchika.
Vilevile, amesema Serikali imetoa vibali vya ajira kwa Mamlaka zote za Serikali za Mitaa Kumb. Na. CFC.26/205/01/PF/91 cha tarehe 22 Agosti, 2017 na kibali Kumb. Na CFC.26/205/01/GG/95 cha tarehe 12 Machi, 2018 kuziba nafasi zote z... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More