SERIKALI INAENDELEA KUIMARISHA USIKIVU WA TBC NCHI NZIMA:DKT.MWAKYEMBE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI INAENDELEA KUIMARISHA USIKIVU WA TBC NCHI NZIMA:DKT.MWAKYEMBENa Shamimu Nyaki –WHUSM.
Katika kuimarisha usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Serikali imeendela kuweka mikakati mizuri ya kuongeza usikivu wa shirika hilo hapa nchini kutegemea na upatikanaji wa fedha.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akijibu swali la mbunge Mhe. Zaynab Matitu Vulli (Viti Maalum) aliyeuliza Ni chanagamoto zipi zinazopelekea TBC kutosikika katika baadhi ya maeneo ya Pwani ambapo Mhe. Waziri alieleza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2016/17 maeneo mengi ya nchi yaliongezewa usikivu.
“TBC ina mitambo ya kurushia matangazo  ya redio ya masafa ya FM katika Wilaya ya Kisarawe ambayo hufikisha matangazo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani katika masafa ya  87.8 MHz kwa idhaa ya TBC Taifa, 90.0 MHzkwa idhaa ya TBC FM na 95.3 kwa idhaa ya TBC International”.Alisema Dkt. Mwakyembe.Aidha ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2016/17 TBC ilitekeleza mradi... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More