SERIKALI INATAMBUA NA KUHESHIMU MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA-WAZIRI UMMY MWALIMU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI INATAMBUA NA KUHESHIMU MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA-WAZIRI UMMY MWALIMU

SERIKALI inatambua na kuthamini juhudi za wadau mbali mbali zinazofanywa zenye lengo la kuhakikisha maendeleo ya Watanzania yanawezeshwa kikamilifu, hasa zinazochochewa na asasi za kiraia. 
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Watoto wa wizara hiyo, Margaret Mussai alipokuwa akifungua Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii ulioandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation.
Akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha asasi mbalimbali za kiraia, alisema Serikali inafarijika kuona wadau wakiungana na kupanga mikakati ya kufikia malengo ya mafanikio ya utendaji kwa pamoja kuihudumia jamii.
“...Asasi za kiraia mmekuwa muhimili muhimu kwenye kuhimiza maendeleo ya jamii, mmekuwa mnabuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha vijana na wanawake kiuchumi na kutoa huduma za maendeleo ya Jamii kwa kutumia gharama nafuu na hata muda mwingine kwa kutumia rasilimali za wanaojitolea,”
“..... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More