SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO

Na Greyson Mwase, Sumbawanga

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo tayari kuwasaidia wawekezaji kwenye shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ili uchimbaji wao ulete manufaa kwa nchi.

Aliyasema hayo leo tarehe 12 Oktoba, 2018 mara baada ya kumaliza ziara yake katika mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited uliopo katika kijiji cha Nkomolo II Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Katibu Tawala Msaidizi – Sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Happiness Shayo, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na waandishi wa habari.

Alisema kuwa katika kuhakikisha watafiti na wachimbaji wa madini wa... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More