SERIKALI KUANZISHA KURUGENZI YA KUSIMAMIA FUKWE KWA AJILI YA UTALII - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI KUANZISHA KURUGENZI YA KUSIMAMIA FUKWE KWA AJILI YA UTALII

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema inatarajia kuanzisha Kurugenzi ya kusimamia fukwe za bahari kwa ajili ya kupanua wigo wa mapato yatokanayo na sekta ya  utalii .
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ameyasema hayo leo  wakati alipotembelea makao makuu ya Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) jijini Dar es Salaam ambapo amezungumza na watumishi wa bodi hiyo na kuwataka wawe wabunifu katika kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi.
Amesema licha ya kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na fukwe nyingi lakini fukwe hizo zimekuwa hazitumiki ipasavyo katika kuliingizia taifa mapato kupitia utalii.
Amefafanua kuwa Kurugenzi hiyo itakayoundwa itakuwa na jukumu la kusimamia fukwe zote nchini ikiwa pamoja na  kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji ili waweze kuziboresha kwa ajili ya watalii wa ndani na nje ya nchi
Pia ametoa wito kwa Wawekezaji wenye nia ya kutaka  kuwekeza kwenye fukwe hizo ambazo zitakuwa zikisimamiwa na Kurugenzi hiyo  waka... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More