Serikali kudhibiti Uhalifu Ukanda wa Ziwa na Bahari - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali kudhibiti Uhalifu Ukanda wa Ziwa na Bahari

Na Mwandishi Wetu
Serikali imejipanga kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kote nchini ili kuweza kudhibiti uhalifu unaotekelezwa majini ikiwepo uvuvi haramu, usafirishaji wa magendo na uhalifu mwingine unaotokea katika maeneo ya ziwa na bahari.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya boti maalumu ya doria na ufunguzi wa Kituo cha Polisi Wanamaji, wilayani Chato, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inadhibiti uhalifu katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kwa kutumia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya serikali, ili kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kuchumi bila ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao
Alisema moja ya changamoto kubwa aliyoelezwa wakati alivyofanya ziara ya awali wilayani Chato ni kuwepo kwa matukio ya uhalifu ziwani yaliyopelekea baadhi ya wananchi kusitisha shughuli za kiuchumi katika mwambao huo wa Ziwa Victoria.
“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiri... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More