Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa

Na: Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.
Serikali imeendelea kuchukua hatua za kubatilisha milki za ardhi za mashamba yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yamesema Bungeni leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mhe. Dustan Kitandula Mbunge wa Mkinga kuhusu kufuta hati za mashamba yaliyotelekezwa.
"Katika kipindi cha Disemba, 2015 mpaka Octoba, 2018 mashamba yenye ukubwa wa ekari 84,240.803 yamebatilishwa katika Halmashauri za Ngorongoro, Arumeru, Moshi, Kinondoni,(Manispaa), Kigamboni(Manispaa), Mvomero, Kilombero, Kilosa, Mvomero, Iringa, Bukoba, Tarime, Kibaha, Serengeti, Busega, Muheza, Lushoto na Mkinga" amefafanua Naibu Waziri Mabula. 
Mabula anasema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Shamba Na. 278 Mkomazi lenye ukubwa wa ekari 15,442 lililokuwa likimilikiwa na kampuni ya M/S Mkomazi Plantations Limited kwa Hati Namba 4268, 9780 na 9781 milki yake ilithibitishwa tarehe 20 Juni, 2018.
Aidha anafafanua ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More