SERIKALI KUPITIA UPYA MKATABA WA UJENZI KITUO CHA FORODHA HOROHORO- TANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI KUPITIA UPYA MKATABA WA UJENZI KITUO CHA FORODHA HOROHORO- TANGA

Na Peter Haule, WFM, TangaSerikali imetoa agizo kwa watendaji wa Kituo cha pamoja cha Forodha Mpakani- Horohoro, kuwasilisha nyaraka za ujenzi wa Kituo hicho ukiwemo mkataba kwa kuwa miundombinu iliyopo haijakidhi viwango jambo lililosababisha kutofunguliwa rasmi kwa kituo hicho tangu mwaka 2015.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro walipofanya ziara ya kutembelea na kukagua Kituo hicho ambapo hawakuridhishwa na miundombinu yake.
Dkt. Kijaji, alisema kuwa Kituo hicho hakina mawasiliano kati ya upande wa Tanzania na Kenya hivyo kutokidhi vigezo vya kuwa Kituo cha pamoja cha Forodha kati ya nchi hizo mbili.
Alisema kuwa ukosefu wa mawasiliano unasababisha urasimu katika kuwahudumia wananchi jambo linalosababisha wateja katika mpaka huo kutafuta njia nyingine ambazo sio rasmi katika usafirishaji bidhaa jambo ambalo linaathari kubwa katika ukusanyaji wa mapato.
Miongon... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More