SERIKALI KUTOVIVUMILIA VYUO VITAKAVYOTOA MAFUNZO KINYUME NA UTARATIBU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI KUTOVIVUMILIA VYUO VITAKAVYOTOA MAFUNZO KINYUME NA UTARATIBU

Na Chalila Kibuda, Globu ya JamiiSERIKALI imesema haitavivumilia  vyuo ambavyo vitabainika vinatoa mafunzo yake kinyume na utaratibu uliowekwa na lengo ni kuhakikisha vijana wanapata elimu bora.
Pia imeiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), kuongeza kasi ya ukaguzi na kuvifungia vyuo hivyo bila kujali ni vya umma au binafsi na kufafanuliwa Serikali hutenga Sh.bilioni 427.5 kwa ajili ya utoaji wa elimu kwa vyuo vya elimu ya juu nchini, hivyo haitarajii kuona madudu yanafanyika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati anafungua maonesho ya 13 ya Vyuo  vya Elimu ya Juu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema Serikali haitaweza kuvumilia uwepo wa vyuo visivyokuwa na sifa nchini kwani vimekuwa ni chanzo vya kuzalisha uwepo wa wanafunzi wasio na sifa.
Prof.Joyce amesema hivi karibuni Serikali  ilifanya ukaguzi kwa baadhi ya vyuo na kubaini kuwepo kwa programu nyingi zilizokuwa zikiendeshwa kinyume cha taratibu.
“Sasa TCU... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More