SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

SERIKALI inatarajia kutumia Shilingi Tirioni 1.3 kupitia mkopo toka Exim benki ya nchini India kwa ajili ya miradi mikakati ya maji katika Miji 28 nchi nzima ili kukabiliana na tatizo la maji. 
Hayo yamebaimnishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara katika mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga-Uwasa) na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo.

Profesa Mkumbo alifanya ziara katika mamlaka hiyo kwa ajili ya kujionea utendaji wa kazi zao na zaidi kuona changamoto zinazowakabili watumishi hao na mamlaka husika na namna ya kuzitafutia ufumbuzi. Profesa Mkumbo alisema katika fedha hizo zaidi ya Shilingi Bilioni 140 zitainufaisha Miji ya Pangani,Muheza na Korogwe ambapo matarajio ya Serikali kuhakikisha kufikia malengo ya asilimia 85 Vijijini na 95 Mijini hadi kufikia 2025.

Alisema katika Miji hiyo Pangani imepangiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 22.5,Muheza Bilioni 5.6 na Korogwe kupitia mradi Mkuu wa maji Korogwe na Handeni ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More