Serikali ya Kenya yaagiza Bar zote zifungwe wikiendi hii, Wakenya wageuka mbogo mtandaoni - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali ya Kenya yaagiza Bar zote zifungwe wikiendi hii, Wakenya wageuka mbogo mtandaoni

Serikali ya Kenya imeagiza kuwa kuanzia Jumamosi Agosti 24 hadi Jumapili Agosti 25, 2019, Bar na kumbi za starehe zote nchini Kenya zifungwe ili kupisha zoezi la Sensa.


Image result for fred matiang'iFred Matiang’i

 


Amri hiyo imetolewa jana Agosti 21, 2019 na Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya, Fred Matiang’i wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mashidano ya michezo mbalimbali yanayoandaliwa na Makampuni ya kutoa huduma ya maji nchini humo, Iliyofanyika katika uwanja wa Embu.


Tunaenda kufunga mahali pote pa kujiburudisha kwanza tutaanza na Bar, Tutafunga kuanzia saa 11 jioni hadi 12 asubuhi ili kukupatia muda wa kuwa nyumbani kabla ya maafisa wa kuhesabu watu kufika majumbani kuanzia saa 12 jioni,” amesema Waziri huyo.


Hakuna mtu atatoka nje ya kijiji chako, kumaanisha kuwa ni watu ambao wanafahamu kila mtu hapa, wanajulikana na wanajua kila mahali,” ameongezea Matiang’i.


Waziri huyo pia, Amewahakikishia Wakenya kuwa hali ya usalama itaimarishwa kwani maafisa wote wa usalama wamezuili... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More