SERIKALI YA ZANZIBAR YAKABIDHI FEDHA ZA FIDIA KWA WANANCHI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YA ZANZIBAR YAKABIDHI FEDHA ZA FIDIA KWA WANANCHI.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekabidhi Fedha za fidia kwa Wananchi waliopisha Ujenzi wa Karantini ya Mifugo katika eneo la Nziwengi katika Jimbo la Gando liliomo ndani ya Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Fedha hizo zilizotolewa na Serikali na Kukabidhiwa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi zimelengwa kwa Wakulima 40 waliokuwa wakiendesha shughuli zao za Kilimo na Mifugo katika eneohilo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa Hekta 60.9.
Akikabidhi fedha hizo kwa Wakulima hao, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema subra iliyofanywa na Wakulima hao wa Jimbo la Gando hatimae imeleta neema itakayowaenea Wananchi wa jimbo hilo hasa wakati huu wa kuelekea kwenye Siku Kuu ya Iddi El – Hajj.
Balozi Seif aliwaasa na kuwakumbusha Wakulima na Wananchi hao wa Gando wawe makini katika matumizi ya fedha walizokabidhiwa kuzilenga kwenye uanzishaji wa shughuli za Kilimo walizokuwa wakizifanya katika maeneo mengine.
“ Nimefarajika kushuhudia kitendo hichi cha... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More