SERIKALI YAAGIZA HATUA KALI KWA WATAKAOINGIZA MAFUTA YA MAGENDO - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAAGIZA HATUA KALI KWA WATAKAOINGIZA MAFUTA YA MAGENDO

Yazitaka mamlaka husika kudhibitiuingizwaji wa vyakula visivyokuwa na virutubisho
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameziagiza kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuhakikisha zinachukua hatua kali dhidi ya watu wote watakaobainika wanaingiza nchini bidhaa za chakula na mafuta ya kupikia kwa njia za magendo. Kadhalika, Waziri Mkuu aziagiza mamlaka husika kuhakikisha zinaendelea kudhibiti uingizwaji holela wa bidhaa mbalimbali za vyakula visivyokuwa na virutubisho yakiwemo mafuta ya kupikia na kutoa adhabu kali kwa wafanyabiashara watakaobainika kuingiza bidhaa hizo nchini. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Novemba 15, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Vullu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma. Mbunge huyo alihoji kuhusiana na suala la uagizwaji wa mafuta ya kupikia kutoka nje kama unazingatia sheria iliyopitishwa na Serikali ambayo inayolazimisha vyakula na mafuta ya kula kuwekwa v... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More