SERIKALI YAANZA KUTUMIA NDEGE KULINDA MISITU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAANZA KUTUMIA NDEGE KULINDA MISITU

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imeanza kutumia safari za anga kufanya doria katika kukabiliana na changamoto kubwa inayoikabili serikali katika uhifadhi wa Sekta ya misitu na maliasili kwa jumla.
Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa TFS Professa Dos Santos Silayo, amesema lengo la doria hizo ni kuhakikisha ulizi unaimarishwa katika maeneo yote ya misitu ambayo TFS imepewa dhamana ya kuilinda.
“Nimeelekeza watendaji wangu kufanya doria ya anga kuanzia leo na tutaanza na Kanda ya Mashariki na nizitake kanda nyingine zijipange, maeneo/misitu korofi myabaini na kutafuta ramani zake. Nitawatumia ndege kwa ajili ya doria kutambua uharibifu.
“Tumekuwa tukifanya doria za misitu lakini tumekuwa tukiwiwa vigumu kuyafikia maeneo yote, lakini kupitia doria za anga sasa tutajua kila kinachoendelea kwenye eneo la misitu na kwa kutumia vikosi kazi vyetu tutafanya ulinzi kwa uhakika zaidi,” amesema Profesa Silayo.
Professa Silayo aliongoza kuwa ili kuonge... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More