Serikali yafikia hatua za mwisho kukamilisha Sera ya Michezo - Dkt. Mwakyembe - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali yafikia hatua za mwisho kukamilisha Sera ya Michezo - Dkt. Mwakyembe

Na Shamimu Nyaki –WHUSMSerikali imefikia hatua za mwisho za kukamilisha rasimu ya Sera ya   Maendeleo ya Michezo baada ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau ndani na nje ya nchi na ni matarajio ya wizara kukamilisha zoezi hili ndani ya muda mfupi.Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge Rashid Shangazi wa Mlalo (CCM) aliyeuliza kuwa ni lini serikali itakamilisha Sera ya Michezo. “Zoezi la kupitia upya Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995 ni zoezi ambalo limehusisha ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa michezo na   tayari rasimu kamili ya Sera hiyo imefikia hatua nzuri.”Alisema Dkt. Mwakyembe.Aidha Mhe. Mwakyembe ameongeza kuwa  Sera ya Michezo itakapokamilika itasaidia kuleta mabadiliko mengi ya kisera ikiwemo kuibuka kwa michezo ya kulipwa,mahitaji ya shule na vyuo mahususi vya michezo mbalimbali  kwa lengo la kulea vipaji toka utot... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More