Serikali yaipongeza Haki Elimu kwa kuinua kiwango cha elimu nchini - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali yaipongeza Haki Elimu kwa kuinua kiwango cha elimu nchini

Na Charles James, Michuzi TV
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Haki elimu, inayojishughulisha na kutoa elimu ya usawa kwa watoto wote katika elimu, limezindua utafiti uliofanyika na kituo hicho katika mikoa mitano(5) kujua changamoto zinazowakwamisha watoto wa kike katika kupata elimu katika Jamii zetu.
Akizindua utafiti huo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia, Dkt Leonard Akwilapo, amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na asasi za kiraia Kama Haki elimu, katika kuinua elimu hapa nchini na serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha watoto hasa wa kike wanabaki shule.
"Sisi Kama serikali tunatambua kazi kubwa mnayoifanya asasi za kiraia, hasa ninyi haki elimu, mnasaidia kueneza elimu kwa Jamii na kuhakikisha watoto wanabaki shule, na sisi serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha watoto hasa wa kike wanabaki shule" amesema, Dkt Akwilapo.
Serikali imekuja na mpango wa elimu bure kwa shule za awali hadi kidato cha nne yote haya ni kuhakikish... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More