SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA MFUMO MADHUBUTI WA KIKATIBA NA KISHERIA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA MFUMO MADHUBUTI WA KIKATIBA NA KISHERIA

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imejipanga kuimarisha mfumo madhubuti wa kikatiba na kisheria ili kufanikisha utekelezaji wa sera na mipango kwa maendeleo ya Taifa.
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) alipokuwa akiwasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
Balozi Mahiga amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha, wizara hiyo itaendelea kuboresha utoaji wa huduma za kisheria kwa Umma ambapo imeainisha maeneo mahususi ya vipaumbele na kuyawekea mikakati ya utekelezaji.
"Ili kufanikisha utekelezaji wa vipaumbele hivyo vitakavyoisaidia nchi kusonga mbele, katika Bajeti ya Mwaka 2019/20 Wizara yangu inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 55,175,163,302 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo", alisema Balozi Mahiga.
Balozi Mahiga amevitaja baadhi ya vipaumbele vya Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo vikiwemo vya k... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More