Serikali yakabidhi Pikipiki 27 kwa Maofisa Elimu Kata Halmashaauri ya Wilaya Mufindi. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali yakabidhi Pikipiki 27 kwa Maofisa Elimu Kata Halmashaauri ya Wilaya Mufindi.


Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekabidhi  Pikipiki ishirini na saba (27) aina ya Honda kwa Maofisa elimu kata  kutoka kata zote ishirini na saba (27)  za Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mkoani Iringa.Akizungumza mara baada ya kukabidhi Pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri David William, amesema Pikipiki hizo zimefika kwa wakati muafaka ili kurahisisha jukumu la ufuatiliaji na usimamizi wa elimu katika Halmashauri.“Mmepata usafiri huu ambao utachangia kutatua changamoto za kufanya kazi zenu hivyo, hatutaki kuona utoro unaendelea, hatutaki kuona mimba zinandelea hasa katika shule za sekondari, sasa hatuna sababu ni lazima tuhakikishe elimu inakua bora zaidi na ufaulu wetu kitaifa kama Halmashauri unapanda” alisema Mhe William.Aidha, Mhe. William, ametoa wito kwa Maofisa elimu kata kuhakikisha wanazitunza Pikipiki hizo na kusisitiza kwamba usafiri huo sio kwa ajili ya kufanyia biashara ya bodaboda bali zifanye kazi iliyokusudiwa.Pikipiki zilizot... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More