Serikali yamkana RC Makonda sakata la kutokomeza ushoga ‘Tanzania itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali yamkana RC Makonda sakata la kutokomeza ushoga ‘Tanzania itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa’

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema kampeni ya kuwasaka watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga inayoratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda ni mawazo yake binafsi na sio msimamo wa Serikali.


“Wizara ya Mambo ya Nje kwa niaba ya Serikali inapenda kuwajulisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya ushoga yaliyoongelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,” imeeleza taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyotolewa jana Jumapili Novemba 4, 2018.


Katika taarifa hiyo, Serikali imekumbusha na kusisitiza kuwa itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo imesaini na kuridhia.


“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba,” imesema taarifa hiyo.Mwanzoni mwa wiki hii RC Makonda alinda Kamati ya watu wasio... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More