SERIKALI YAOMBWA KUWEKA UWIANO WA WANAFUNZI WENYE UFAULU DARAJA LA KWANZA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAOMBWA KUWEKA UWIANO WA WANAFUNZI WENYE UFAULU DARAJA LA KWANZA


Na Jusline Marco:Arusha
Serikali imeombwa kuweka uwiano wa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza katika shule zote za elimu ya juu ili kuleta motisha kwa wanafunzi wanaojiunga na masomo kwenye shule hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa shule ya sekondari ya Mwandeti iliyopo katika kata ya Mwandeti,Wilayani Arumeru Mkoani Arusha kufuatia shule hiyo kushika nafasi ya nne kitaifa na nafasi ya pili kimkoa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.
Amesema kuwa pamoja na shule hiyo kutoa wanafunzi 70 wenye ufaulu wa daraja la kwanza na wanafunzi 6 wenye ufaulu wa daraja la pili jitihada kubwa zimetumika ili kufanikisha shule hiyo inafanya vizuri zaidi kwani wengi wao walijiunga wakiwa na ufaulu wa daraja la tatu na daraja la pili katika matokeo ya kidato cha nne.
Vilevile ameeleza kuwa kushika kwa nafasi hiyo kunatokana na jitihada kubwa zilizofanyika na uongozi wa shule hiyo kwa kushirikiana na walimu wao kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji pamoja na kufanya ziara za... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More