Serikali Yaondoa Zuio La Kuuza Mazao Nje Ya Nchi - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali Yaondoa Zuio La Kuuza Mazao Nje Ya Nchi


Na Stella Kalinga, SimiyuRais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa amesema Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi  ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini.
Mhe. Mkapa amesema hayo katika Kilele  cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu,  Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi ambapo alikuwa mgeni Rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
“Ninachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi    ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini, hata hivyo mazao hayo yatauzwa nje ya nchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu”alisema.
Aidha,  amesema Serikali inawakumbusha wananchi wote kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula wakati wa kuuza mazao yao ili kujihakikishia usalama wa chakula katika kaya zao.
Mkapa pia amesema Seri... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More