SERIKALI YAONDOA ZUIO LA KUUZA MAZAO NJE YA NCHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAONDOA ZUIO LA KUUZA MAZAO NJE YA NCHI

Na Stella Kalinga, Simiyu
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa amesema Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini.
Mhe. Mkapa amesema hayo katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambapo alikuwa mgeni Rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
“Ninachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini, hata hivyo mazao hayo yatauzwa nje ya nchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu”alisema.
Aidha, amesema Serikali inawakumbusha wananchi wote kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula wakati wa kuuza mazao yao ili kujihakikishia usalama wa chakula katika kaya zao.Mkapa pia amesema Serikali i... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More