SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KWA MADAKTARI KUWAANDIKIA WAGONJWA DAWA KWA MAJINA YA KIBIASHARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KWA MADAKTARI KUWAANDIKIA WAGONJWA DAWA KWA MAJINA YA KIBIASHARA


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.  Serikali imepiga marufuku kwa madaktari kuwaandikia wagonjwa dawa kwa majina ya kibiashara badala yake watumie majina ya asili (Generic name). Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua mkutano wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.  Dkt. Ndugulile amesema imefika wakati serikali imebidi kutoa tamko hilo kwasababu Madaktari wengi wamekuwa wakikiuka miongozo wa utoaji matibabu uliotolewa na wizara ya afya. "Katika mfumo wa utoaji wa huduma za afya, tunamtaka daktari aandike kwa jina la asili ili mfamasia akatafsiri aina ile ya dawa tulizonazo kwenye akiba yetu za dawa tulizonazo, ubora wa dawa za Tanzania ni za kiwango cha juu kabisa, tuwaambie wa Tanzania waache zile dhana potofu akisikia zile zinazotoka," amesema.  Amesema kinacho... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More