SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WATUMISHI WA UMMA WALIOHAMIA DODOMA KUOMBA UHAMISHO KUREJEA DAR ES SALAAM - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WATUMISHI WA UMMA WALIOHAMIA DODOMA KUOMBA UHAMISHO KUREJEA DAR ES SALAAM


Serikali imepiga marufuku Watumishi wa Umma waliohamia Makao Makuu ya Nchi Dodoma kwa gharama za Serikali kuomba uhamisho wa kurejea jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusiana na zoezi zima la uhamisho wa watumishi wa umma kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Dkt. Ndumbaro amesema kuwa,  Ofisi yake imekuwa ikipokea barua mbili au tatu kwa siku za watumishi waliohamia Dodoma kuomba uhamisho wa kurejea Dar es Salaam kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kiafya wakati hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa ina vifaa vya kisasa na uwezo mkubwa wa kutoa huduma za matibabu kwa watumishi hao.
Dkt. Ndumbaro amefafanua kwamba,  kabla ya watumishi kuhamia Dodoma, Serikali ilitoa maelekezo kwa waajiri kuwasilisha orodha ya watumishi wenye matatizo ya kimsingi ili wabaki kwenye ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More