Serikali yasema upatu ni haramu, yawaonya wanaofanya biashara hiyo - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali yasema upatu ni haramu, yawaonya wanaofanya biashara hiyo

Na Peter Haule, WFM, DodomaSerikali imewaonya wanaofanya biashara ya upatu (Pyramid Scheme) kwa kuwa sio halali na hakuna taasisi wala mtu binafsi aliyepewa leseni ya kufanya biashara hiyo.Onyo hilo limetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (pichani), wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Munira Mustafa Khatib, aliyetaka kujua ni lini Serikali itadhibiti biashara za upatu ambazo zimekuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Taifa.Dkt. Kijaji alisema kuwa,  kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, biashara ya upatu ni haramu na huendeshwa kinyume na sheria na taratibu za nchi hivyo Serikali huchukua hatua dhidi ya wahusika kama ilivyofanya kwa taasisi ya DECI.
“Washiriki wa biashara ya upatu na wale wanaoshawishi ufanyaji wa biashara hiyo, wote wanatenda kosa na wanatakiwa kupata adhabu na sio kusaidiwa na Serikali”, alieleza Dkt. Kijaji.Alisema kuwa Serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya biashara ya upatu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More