SERIKALI YASISITIZA WAFUNGWA KUTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YASISITIZA WAFUNGWA KUTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amekabidhi mashine 10 za kufyatulia matofali kwa jeshi la magereza la mkoa wa Lindi na kuwataka kuzitumia ipasavyo ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwemo makazi duni.

Mashine hizo ni sehemu ya ahadi aliyoitoa mwaka mmoja na nusu uliopita baada ya kufanya ziara katika mkoa wa Lindi. Masauni alikabidhi mashine hizo katika gereza la Lindi mjini mkoani hapa na kuwataka jeshi la magereza kujipanga ipasavyo namna ya kuzitumia ili ziwe na tija na manufaa kwao.

Alisema mwaka uliopita alifanya ziara ya kukagua shughuli za magereza na kukutana na changamoto mbalimbali ikiwamo makazi duni ya nyumba za udongo hasa katika gereza la Lindi Mjini. “Nawakabidhi mashine hizi leo, natarajia kuona mabadiliko yenye tija kutoka kwenu. Mkifanya vizuri nitawatafuta wadau wengine kwa ajili ya kuongeza mashine hizi,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;

“Nataka gereza la Lindi Mjini liwe la mfano kwa magereza ya mkoa hu... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More