Serikali Yatoa Bilioni Moja kwa Timu ya Taifa - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali Yatoa Bilioni Moja kwa Timu ya TaifaRais wa shirikisho la soka nchini Kenya (FKF), Nick Mwendwa, ameweka wazi kuwa serikali ya Kenya inaanza utekelezaji wa ahadi yake ya kuwekeza zaidi ya shilingi 240 milioni zaidi ya bilioni tano za Tanzania kwenye michezo.

Mwendwa amesema Serikali imethibitisha kuwa wiki ijayo itaikabidhi timu ya taifa ya mpira wa miguu (Harambee Stars) kiasi cha shilingi milioni 50 za Kenya, zaidi ya bilioni moja za Tanzania ikiwa ni sehemu ya ahadi ambayo ilitolewa na serikali kupitia kwa makamu wa Rais William Ruto.

Rais Mwendwa amesema pesa hizo zitatumika kutekeleza shughuli za soka, ikiwa ni pamoja na kuandaa timu kwaajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 zinazofanyika Misri.

"Mpaka wiki ijayo wachezaji wakiripoti kambini tuna uhakika pesa zitakuwa kwenye akaunti yetu na tutawapatia wagawane wenyewe kwa usawa kisha sisi tuendelee na maandalizi ya fainali hizo'', amesema Mwendwa.

Aidha Mwendwa amefafanua kuwa wachezaji wa Harambee Stars watapata milioni 35 za Kenya, zaidi ya milioni 700 za T... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More