Serikali yatoa siku nne kwa wanunuzi wa korosho ‘hatutawaruhusu tena kununua’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Serikali yatoa siku nne kwa wanunuzi wa korosho ‘hatutawaruhusu tena kununua’

Serikali imetoa siku nne kwa wanunuzi wote 35 waliojiandikisha kununua korosho wawe wamepeleka barua katika Ofisi ya Waziri Mkuu wakionesha kiasi cha tani wanazohitaji na lini watazichukua.
“Hivyo wanunuzi waliojiandikisha wakiwemo na wale wote ambao wamekuwa wananunua kwenye minada lakini kwa kiasi kidogo, wahakikishe ndani ya siku hizo nne kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu saa 10 alasiri wawe wameleta barua na ofisi yangu ipo wazi saa 24.”


Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Novemba 9, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu ununuzi wa zao la korosho, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.Baada ya kupita siku hizo Serikali italazimika kufuta usajili kwa wote waliojisajili kununua zao hilo kwa sababu walikubaliana kwenda kununua lakini hali inayoonekana sasa ni kama kumkomoa mkulima kitu ambacho imesema haitakubaliana nacho.


“Mwenye nia ahakikishe katika siku hizo nne iwe ndio mwisho wa kununua korosho na waandike barua kwani ofisi yangu ipo wazi saa 24... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More