SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA UBORESHAJI UPATIKANAJI DAWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA UBORESHAJI UPATIKANAJI DAWA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SERIKALI imezindua mfumo wa kitaifa wa uboreshaji upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupitia mshitiri(Mzabuni binafsi).

Mfumo huo maarufu kwa jina la Jazia unalenga kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinavyokosekena Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ili kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya katika vituo vya tiba.

Mfumo huo umezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Suleiman Jaffo ambapo amesema unakwenda kusaidia kuondoa changamoto ya kukosekana kwa dawa na vifaa tiba katika vituo vya tiba.

"Mfumo huu wa uboreshaji upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupitia mshitiri kutaongeza kasi ya upatikanaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ili kupunguza muda wa kusubiri huduma na kupatikana kwa bidhaa za afya wakati wote,"amesema Jaffo.

Ameongeza mfumo huo ambao umezinduliwa rasmi leo utakuwa ni wa nchi nzima na kutoa maagizo kwa mikoa yote nchini kujiunga na mfumo huo na ifikapo Oktoba ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More