SERIKALI YAZISHAURI BENKI NCHINI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SERIKALI YAZISHAURI BENKI NCHINI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA

Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezitaka Benki nchini kushusha viwango vya riba za mikopo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi wakiwemo wakulima kunufaika na huduma za kifedha zinazotolewa na taasisi hizo za fedha kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua rasmi Tawi la Benki Azania, Sokoine, na kusisitiza kuwa Benki zina nafasi kubwa wa kuisaidia nchi kufikia azma yake ya kuwa ya viwanda ifikapo mwaka 2025 kwa kukuza mitaji na biashara za wananchi.
Alisema kuwa hivi karibuni Serikali imechukua hatua madhubuti za kiutawala na kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo katika soko zinapungua, ikiwemo Benki Kuu kutoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara, kushusha riba kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0.
"Tumepunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za biashara kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0, hatua ambazo zimesaidia kupunguza riba katika ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More