SHAABAN IDDI CHILUNDA APATA MAPOKEZI MAKUBWA CD TENERIFE…APELEKWA HADI UWANJANI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHAABAN IDDI CHILUNDA APATA MAPOKEZI MAKUBWA CD TENERIFE…APELEKWA HADI UWANJANI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Iddi Chilunda leo amepata mapokezi mazuri katika klabu yake mpya, CD Tenerife ya Daraja la Kwanza nchini Hispania anayojiunga nayo kwa mkopo wa miaka miwili kutoka Azam FC.
Chilunda amewasili leo na kupokewa na mashabiki kadhaa wa timu hiyo sambamba na kundi kubwa la Waandishi wa Habari waliomfanyia mahojiano makao makuu ya klabu, Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary.
Akizungumzia mapokezi hayo, Chilunda aliyepelekwa hadi Uwanja wa Heliodoro Rodríguez López, unaotumiwa na timu hiyo amesema; “Kwa kweli nimefurahi sana, yamekuwa mapokezi makubwa ambayo sikuyatarajia. Namshukuru sana Mungu, hii inanipa ujumbe kwamba nina deni kubwa hapa. Watu wana matarajio makubwa na mimi. Nitajitahidi kwa uwezo wa Mungu,”amesema.
Shaaban Iddi Chilunda (kulia) akiwa makao makuu ya CD Tenerife leo
Shaaban Iddi akionyeshwa Uwanja wa Heliodoro Rodríguez López wa CD Tenerife

Shaaban Iddi akizungumza na Waandishi ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More