SHAABAN IDDI CHILUNDA AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA MWISHO WA MSIMU LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHAABAN IDDI CHILUNDA AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA MWISHO WA MSIMU LIGI KUU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa Azam FC ya Dar es Salaam, Shaaban Idd Chilunda amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Mei wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara.
Chilunda alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Jacob Massawe wa Ndanda na Edward Shija wa Kagera Sugar katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na kamati ya tuzo hizo.
Chilunda aliisaidia Azam akifunga mabao 6 kwa mwezi huo, ambapo kati ya mabao hayo matatu ‘hat trick’ alifunga katika mchezo mmoja. 

Shaaban Idd Chilunda amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Mei wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara

Kwa mwezi huo Azam ilicheza michezo minne na kupata pointi tisa, baada ya kushinda michezo mitatu na kufungwa mmoja ikibaki katika nafasi yake ya pili na hakuwa na kadi yoyote.Kwa upande wa Shija aliisaidia Kagera Sugar kupata pointi 10, akifunga mabao matatu katika michezo minne iliyocheza timu yake, ikishinda mitatu na kutoka sare mmoja na kupanda kutoka nafasi ya 12 iliyokuwepo mwezi April... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More