Shabiki aswekwa rumande wiki 14, ni baada ya kumshambulia mchezaji uwanjani - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Shabiki aswekwa rumande wiki 14, ni baada ya kumshambulia mchezaji uwanjani

Shabiki aliyemshambulia kiungo wa klabu ya Aston Villa, Jack Grealish ameswekwa rumande wiki 14 ambayo ni sawa na miezi mitatu na wiki mbili.

Hukumu hiyo imetolewa hii leo siku ya Jumatatu baada ya shabiki huyo aliyetambulika kwa jina la Paul Mitchell mwenye umri wa miaka 27 kumshambulia kwa nyuma mchezaji wa Aston Villa, Jack Grealish wakati wa mchezo wa Championship Birmingham City.

Mbali ya kifungo hicho cha miezi 14 jela lakini pia amefungiwa kutohudhuria viwanjani kwa miaka 10.

Grealish ambaye anaingiza kiasi cha pauni 25,000 kwa wiki amepewa pauni 100 kutokana na kusababishiwa maumivu.

Hata hivyo familia ya Mitchell ilikuwepo mahakamani hapo wakati hukumu hiyo ikitolewa.  

Kiungo huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka Grealish 23 alipigwa kwa nyuma na Mitchell dakika chache tu baada bao wakati wa derby hiyo dhidi ya Birmingham City.


The post Shabiki aswekwa rumande wiki 14, ni baada ya kumshambulia mchezaji uwanjani appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More