Shaffih Dauda alivyochungulia uhamisho wa Ronaldo kwa jicho la biashara - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Shaffih Dauda alivyochungulia uhamisho wa Ronaldo kwa jicho la biashara

Uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid kwenda Juventus ni uhamisho ambao unaangaliwa kwa angle ya 360, ukiuangalia kwa kawaida utakufanya uumie utashindwa kufikiria ni aina gani ya biashara imefanyika.


Ukifatilia kwa dunia ya sasa hivi ambayo mpira wa miguu umehamia pia nje ya uwanja, uhamisho huu wa Ronaldo unagusa sehemu nne ambazo mmoja utaathirika mwingine unapata faida lakini mwisho wa siku ilibidi uhamisho ufanyike ili upande ambao tunaona utapata hasara tuone kama hasara itatokea.


Uhamisho huu unamgusa mwenyewe mchezaji, unagusa klabu ya Real Madrid, unagusa klabu ya Juventus, na unagusa Seria A pamoja na La Liga kwa sababu uhamisho wa mchezaji una athari pia kwenye ligi.Kama unakumbuka kipindi kile Neymar anakwenda ligi ya Ufaransa kulikuwa na vita kubwa sana kati ya bodi ya ligi ya La Liga ambao hawakuwa tayari kumshuhudia Neymar anaondoka kwenye ligi yao kwenda ligi nyingine matokeo yake anakwenda kuipa nguvu ligi nyingine na wao wanashindana wanataka La Liga ibak... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More