Shaffih Dauda atoa ya moyoni kuhusu nafasi ya uraisi wa Simba - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Shaffih Dauda atoa ya moyoni kuhusu nafasi ya uraisi wa Simba

Wakati habari ya raisi wa Simba Salim Abdallah kutogombea tena uongozi katika klabu hiyo zikiendelea kutawala, mchambuzi wa masuala ya soka Shaffih Dauda amesema haya kuhusu uamuzi wa Salim.


“Salim Abdallah aliingia kukaimu nafasi ya urais wakati viongozi wa Simba wamepata matatizo kwa hiyo wakati akikaimu ndio ikaja hiyo hoja ya mabadiliko na yeye akapitisha mchakato wa mabadiliko ambalo ndio lilikuwa jukumu lake kuhakikisha anasimamia katika kipindi cha mpito cha mchakato hadi watakapofika kwenye kipindi cha uchaguzi ambapo nafasi ya kukaimu itakwisha.


Sio hilo tu, wakati akikaimu Simba pia ilikuwa na matokeo bora uwanjani ambayo walikuwa wameyakosa kwa muda mrefu ndio maana watu wengi wakataka achukue fomu wamchague aendelee kuongoza.


Kwa mara ya kwanza naona kiongozi wa mpira ambaye alikuwepo madarakani watu wanamlilia aendelee kuwepo lakini yeye anaamua kukaa pembeni.


Hapa tunajifunza kwamba, kuna watu ambao wapo nje ya uongozi lakini wana uwezo. Hili ni fundisho kwa wanachama k... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More