SHAHIDI KESI YA MALINZI ASEMA; “TULIKUBALI KUBADILI WATIA SAINI TFF BAADA YA KUJIRIDHISHA TARATIBU ZILIFUATWA” - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHAHIDI KESI YA MALINZI ASEMA; “TULIKUBALI KUBADILI WATIA SAINI TFF BAADA YA KUJIRIDHISHA TARATIBU ZILIFUATWA”

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MENEJA wa benki ya Stanbic tawi la Centre Kinondoni mjini Dar es Salaam, Adelhem Msiagi amesema kwamba walikubali mabadiliko ya watia saini wa akaunti za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kujiridhisha taratibu zilifuatwa.
Msiagi ameyasema hayo leo Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu mjini Dar es Salaam baada ya kesi inayowakabili vigogo watano wa TFF, akiwemo aliyekuwa Rais, Jamal Malinzi na Katibu wake, Celestine Mwesigwa  kuanza kusikilizwa leo.    
Akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, Msiagi aliiambia Mahakama kwamba TFF ni wateja wao kwa sababu wana akaunti sita katika benki yao ambazo watia saini wake ni sita pia. 

Kesi ya vigogo wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) na Selestine Mwesigwa (kulia) imeanza kusikilizwa leo

Kimaro alianza kwa kuwakumbusha washitakiwa hao, mashitaka 30 yanayowakabili kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa na ndipo shahidi huyo alisema maju... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More