Shamimu na Mumewe, waendelea kusota Rumande - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Shamimu na Mumewe, waendelea kusota Rumande

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Abdul Nsembo maarufu Abdulkandida (45) na mkewe, Shamim Mwasha (41), bado inasubiri majibu ya kielelezo kutoka kwa mkemia mkuu wa Serikali ya Tanzania.


Hayo yameelezwa na wakili wa Serikali, Simon Wankyo leo Jumatatu Julai 8, 2019 mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa kinachosubiriwa ni majibu ya kielelezo kutoka kwa mkemia huku akiomba tarehe nyingine ya kutajwa.


Juni 24, 2019 upande wa mashtaka pia ulisema kesi hiyo inasubiri ripoti ya mkemia huyo.


Wakili wa utetezi, Hajra Mungula amedai washtakiwa wako ndani na hawana dhamana na kuutaka upande wa mashtaka kufuatilia kielelezo hicho ili majibu yapatikane kwa wakati.


Hakimu Mhina baada ya kusikiliza maelezo ya hayo ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 22, 2019 kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.


Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog 8020 Fashion na mumewe wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019Tweet... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More