SHEIKH WA MKOA DAR ASHAURI WALIOFUNGA NDOA KUELEKEA MWEZI WA RAMADHANI WASIBEZWE, BALI WAPEWE MOYO KWANI NI JAMBO JEMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHEIKH WA MKOA DAR ASHAURI WALIOFUNGA NDOA KUELEKEA MWEZI WA RAMADHANI WASIBEZWE, BALI WAPEWE MOYO KWANI NI JAMBO JEMA

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema vijana wa Kiislamu ambao wamefunga ndoa wakati wa kuelekea mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wanatakiwa kupongezwa na kupewa moyo badala ya kuwabeza na kuwakejeli kwa uamuzi wao wa kufunga ndoa.
Sheikh Alhad ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao umeanza leo kwa waumini wa dini hiyo kuanza kutekeleza moja ya nguzo za Kiislamu.
Hivyo wakati anazungumza mfungo huo, waandishi wa habari walitaka kupata maoni yake ni kwanini ndoa nyingi zinafungwa wakati wa kuelekea mwezi wa Ramadhan ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua ndoa ni kitu kitukufu na hakuna sababu ya kuwabeza wanaofunga ndoa.
"Kwanza kabisa naoMba muheshimu kitu kinaitwa ndoa kwani ni kitu cha heshima sana na binadamu anapotaka kuongeza nasaba yake lazima itapatikana kupitia ndoa.Ifahamike kuna ndoa na tendo la ndoa na yule ambaye anafanya tendo la ndoa bila ndoa hana tofauti ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More