Sherehe za uzinduzi wa uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Sherehe za uzinduzi wa uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu unaojengwa na halmashauri ya wilaya ya Ruangwa na amezitaka wilaya nyingine kuiga mfano huo.Uwanja huo unaoitwa Majaliwa umezinduliwa kwa mechi kati ya timu ya wilaya ya Ruangwa ya Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza na timu ya Simba SC ya Dar es Salaam, ambayo ndio mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, 2018/2019.Waziri Mkuu amezindua uwanja huo leo (Jumamosi, Agosti 11, 2018), ambapo ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Ruangwa na wananchi kwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi huo.Uwanja huo unajengwa katika kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea na ndio utakaokuwa unatumiwa na timu ya Namungo FC kuchezea mechi za nyumbani.Amesema suala la ujenzi wa uwanja ni jambo muhimu na hata Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linahamasisha ujenzi wa uviwanja katika ngazi za mikoa na wilaya ili kutoa fursa kwa wananchi hususani vijana kushiriki katika michezo, hivyo amezitaka halmashauri nyingine ziige mfano wa wilaya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More