Sheria mpya ya FIFA kuhusu wachezaji wa mkopo, mtihani kwa Chelsea - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Sheria mpya ya FIFA kuhusu wachezaji wa mkopo, mtihani kwa Chelsea


FIFA inataka kuweka sheria mpya inayohusiana na kuzuia idadi kubwa ya timu kutoa wachezaji kwa mkopo. Chelsea mpaka sasa inacheza takribani 40 waliopo kwa mkopo vilabu mbalimbali 2018/19

 

FIFA wana mpango wa kuweka sheria ambayo itaweka kiwango maalum kwa vilabu kutoa wachezaji kwa mkopo au idadi ya muda wa mchezaji kutolewa kwa mkopo.


Hili sakata limekaaje?


Kama unavyojua kuna baadhi ya vilabu vina tamaa ya wachezaji. Wamekuwa na wachezaji wengi sana ambao wanshindwa kuwatumia na mwisho wa siku wanakuwa wanatolewa kwa mkopo tu.


Sheria hiyo imekaaje?


Inasemekana kuwa sheria hiyo itaweka bayana kwamba wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 watatolewa vipi?Mapendekezo ya FIFA ni yapi? 


Mapendekezo ya FIFA ni kwamba mchezaji mwenye miaka 21 kurudi nyuma ambaye amelelewa na klabu yake ya nyumbani na amekuwa akitumiwa na timu yake kwa makataba;
Ataruhusiwa kutolewa na mkopo muda wowote bila kuangalia idadi kwamba ametoka mara ngapu.
Lakini mchezaji ambaye hajacheza timu ya wakubwa na hana mkataba wa kuitumikia timu ya wakubwa basi watatolewa kwa kiwango maalumu.Michy Batshuayi yupo Valencia

Kipa wao Matej Delac, 26, ametolewa kwa mkopo mara 10. FIFA wanataka kudhibiti suala hilo pia la mchezaji kutolewa kwa mkopo mara nyingi.Matej Delac amekuwa mchezaji Chelsea miaka 8 lakini muda wote amekuwa akitolewa kwa mkopo tu
Halafu itakuwaje? 
FIFA wanataka kuweka idadi ya muda kwa mchezaji kutolewa kwa mkopo pia. Tumeona hapo juu Sakata la Mateja ametolewa kwa mkopo mara 10. FIFA wanata kuondoa mchezo huo kwani unaonekana ni kama unadumaza kiwango cha mchezaji.

Raisi anasemaje?


FIFA kupitia raisi wake  Gianni Infantino


” Ni vyema tukaweka sheria za kudhibiti suala hili la mkopo kwa wachezaji. Tunapaswa tuweke sheria za vikosi na idadi ya kutoa wachezaji kwa mkopo” 


Inaonekana raisi anataka kila klabu iwe na idadi maalumu ya wachezaji ambao wana mkataba na timu.


Chelsea hivi karibuni imetoa wachezaji kama Tiemoue Bakayoko (24), Kurt Zouma (23) anaMichy Batshuayi (24).


Juventus pia ni klabu ambayo ina idadi kubwa ya wachezaji waliotolewa kwa mkopo (26)


Source: Shaffih DaudaRead More